13 Aprili 2015 - 09:12
 Uchaguzi wa rais waanza leo Sudan

Uchaguzi wa siku tatu wa rais na mabunge ya taifa na majimbo unaanza hii nchini Sudan.

Uchaguzi wa siku tatu wa rais na mabunge ya taifa na majimbo unaanza hii nchini Sudan. Rais Omar Hassan al-Bashir anatazamiwa kurefusha utawala wake wa miaka 25. Vyama vikuu vya upinzani vinaususia uchaguzi huo, lakini kuna wapinzani 15 wanaogombea urais. Rais Bashir anatakiwa na mahakama ya kimataifa ya uhalifu, kuhusiana uhalifu wa kivita katika jimbo la magharibi la Darfur.